UCHUNGUZI WA STIARI KATIKA RIWAYA YA UHASAMA KILIMANI NA RIWAYA YA UCHUNGU WA MWARIDI
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu ni kuchanganua matumizi ya sitiari katika Riwaya ya Uhasama Kilimani na Riwaya ya Uchungu wa Mwaridi.Malengo mahususi ya utafiti huu ni kubaini utokeaji wa sitiari mbalimbali katika riwaya ya Uhasama Kilimani na Riwaya ya Uchungu wa Mwaridi. Pia Kutathimini mchango wa stiari katika uendelezaji wa ujumbe katika riwaya ya Uhasama Kilimani na Uchungu wa Mwaridi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani na ulifanyika katika maktaba ya chuo kikuu cha Makerere kwasababu ndiyo ina vitabu mbalimbali na mazingira bora pakusomea Utafiti huu umegundua kuwa riwaya hizi mbili zinatumia aina za sitiara kama vile chakavu, mseto,radidifu na sahili. Tunapendekeza kwamba wahakiki wengine washughulikie vipengele vingine kama vile wahusika, usimulizi wa , mandhari, nadharia kama ya umaksi, umuundo na dhamira ya mwandishi wa vitabu hivi.Suala la utafiti ni,”mtafiti Lonyce Wakesho alitafiti uchunguzi wa tashibiha,isitiara na taashira katika Diwani ya Damu Nyeusi”, Kutofautiana na mtafiti huyu , utafiti huu inachunguza matumizi ya stiari katika riwaya ya Uhasama Kilimani na riwaya ya Uchungu wa Mwaridi.