Kuchanganua taswira na Nafasi ya mwanamke mkaa nyumba katika ngano za waswahili.
Abstract
Utafiti huu ulihusu mada kuchunguza taswira na nafasi ya mwanamke mkaa nyumba katika ngano za kijamii ya waswahili. Mwanamke ni kiumbe cha kike ambacho kinaaminiwa kuwa kiumbe cha mwanaume na ambacho kinahitajika kubeba mimba/kuzaa watoto na kuwalea. Ili kutekeleza utafiti huu, nilichunguza na nikaangazie jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika ngano za kijamii ya waswahili . Utafiti huu ulifanywa kwa kukutana na wazee wa Jamii ya waswahili ambao wana maarifa kuhusu huu utafiti na Pia ambapo niliwahoji.